APRILI 1, 2022
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Sergey Belousov Anatetea Jina la Mungu
Aprili 14, 2022, Mahakama ya Jiji la Seversk katika Eneo la Tomsk ilimhukumu Ndugu Sergey Belousov kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Mfuatano wa Matukio
Julai 14, 2020
Maofisa wa FSB walivamia nyumba saba, kutia ndani nyumba ya Sergey. Mpelelezi mmoja wa serikali alijifanya anapendezwa na hivyo akarekodi kisiri mkutano wa kutaniko miezi michache kabla ya uvamizi
Machi 25, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Sergey
Machi 30, 2021
Sergey alishtakiwa kwa kutegemea taarifa za mpelelezi wa serikali. Sergey alishtakiwa kwa kushiriki utendaji wa kidini kwa njia ya video mtandaoni na pia kwa sababu ya kuimba na kusali kwa Yehova Mungu
Maelezo Mafupi Kumhusu
Kama Sergey, kadiri tunavyolisifu jina la Yehova, tunahakikishiwa kwamba “ataikweza nguvu ya watu wake.”—Zaburi 148:13, 14.