AGOSTI 3, 2021
URUSI
Ndugu Andrey Okhrimchuk Anategemea Nguvu za Yehova
Mfuatano wa Matukio
Oktoba 4, 2021
Mahakama ya Eneo la Rostov ilikataa ombi la rufaa la Andrey. Hukumu yake ya awali itaendelea kutumika. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu
Agosti 2, 2021
Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyoko Rostov-on-Don ilimhukumu Ndugu Andrey Okhrimchuk kifungo cha nje cha miaka minne.
Aprili 5, 2021
Kesi ya uhalifu ilianza kusikilizwa
Oktoba 29, 2020
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa. Alishtakiwa kushiriki mikutano ya kidini kinyume cha sheria na kuunga mkono utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Mei 22, 2019
Maofisa wa usalama walifanya upekuzi mapema asubuhi katika nyumba na gari la Andrey
Maelezo Mafupi Kumhusu
Imani yenye nguvu ambayo ndugu na dada zetu nchini Urusi wanaonyesha ni mfano mzuri kwetu sote. Tunajua kwamba Andrey na familia yake watafaulu kuvumilia jaribu hili wanapoendelea kumtegemea Baba yetu wa mbinguni, Yehova.—Zaburi 37:5.