Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo Ya Familia

Mazungumzo Ya Familia

TUNAWEZA KUJIFUNZA NINI KUTOKANA NA . . .Abrahamu?

JE, UNAFIKIRI NI MUHIMU KUWATENDEA WENGINE KWA FADHILI?

• Paka rangi picha hizi. • Soma mistari ya Biblia iliyoonyeshwa, na uieleze unapojaza maneno ambayo yamekosekana. • Tafuta vitu vilivyofichika: (1) mjusi na (2) kisu.

Abrahamu alifanya mambo gani ya fadhili ili wengine wajihisi wamestarehe?

DOKEZO: Mwanzo 18:2, 4-5.

Unaweza kufanya nini ili kuwaonyesha wengine fadhili?

DOKEZO: Waroma 12:13.

Unajifunza nini kutokana na simulizi hili la kitabu cha Mwanzo?

Una maoni gani?

Ni akina nani hasa ambao tunapaswa kujitahidi kuonyesha fadhili?

DOKEZO: Wagalatia 6:10.

Kusanya na Ujifunze

KADI YA BIBLIA 24 SAMSONI

MASWALI

  1. A. Baba ya Samsoni aliitwa ________.

  2. B. Samsoni alionyeshaje nguvu zake kuhusiana na jiji la Gaza?

  3. C. Ni nani aliyemsaliti Samsoni?

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Mwamuzi aliyepigania taifa la Israeli kwa miaka 20. (Waamuzi 15:20) Yehova alimtumia Samsoni ili ‘kuongoza katika kuokoa Israeli kutoka mkononi mwa Wafilisti.’ (Waamuzi 13:5) Roho ya Mungu ilimpa Samsoni nguvu nyingi. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Samsoni alikuwa na imani yenye nguvu katika Yehova.—Waebrania 11:32-34.

MAJIBU

  1. A. Manoa.​—Waamuzi 13:8, 24.

  2. B. Alibeba lango la jiji, miimo yake, pamoja na pingo zake na kuichukua hadi kwenye kilele cha mlima ulio mbele ya Hebroni.—Waamuzi 16:2, 3.

  3. C. Delila.​—Waamuzi 16:4, 5.

Watu na Nchi

 Majina yetu ni Lesly, Cathleen, na Alondra. Nina umri wa miaka 10, Cathleen ana umri wa miaka 8, na Alondra na umri wa miaka 7. Tunaishi Mexico. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Mexico? Ni 295,400, 455,000, au 724,700?

Ni alama gani inayoonyesha eneo tunaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, chora alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Mexico.

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Majibu

  1.  Mjusi katika picha ya 5.

  2.  Kisu katika picha ya 2.

  3.  724,700.

  4.  A.