Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

Italia

Katika mwaka wa 2011 nchini Italia, baiskeli zilinunuliwa kwa wingi kuliko magari. Miongoni mwa sababu zilizotajwa ni kuzorota kwa uchumi, kupanda kwa gharama za mafuta, na gharama za udumishaji wa magari. Kwa upande mwingine, ni rahisi zaidi kudumisha na kutumia baiskeli.

Armenia

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu imeamua kwamba serikali ya Armenia ilikiuka haki za vijana 17 ambao ni Mashahidi wa Yehova, waliokamatwa kwa sababu ya kukataa kufanya utumishi wa kiraia unaosimamiwa na jeshi. Mahakama hiyo iliamuru serikali iwalipe ridhaa vijana hao na pia kulipia gharama za kesi.

Japani

Asilimia 63 ya watoto walioathiriwa na uhalifu unaofanywa kupitia vituo vya mawasiliano hawakuwa wameonywa na wazazi wao kuhusu hatari za vituo hivyo. Katika visa 599 vilivyochunguzwa, asilimia 74 ya watuhumiwa wa uhalifu huo walikiri kwamba lengo lao lilikuwa kufanya ngono na watoto.

China

Ili kupunguza tatizo la msongamano, miji mikubwa nchini China inapunguza idadi ya magari mapya yanayosajiliwa. Kwa mfano, mji wa Beijing utasajili magari yasiyozidi 240,000 kwa mwaka. Mnamo Agosti 2012, watu wapatao 1,050,000 walishiriki bahati-nasibu iliyotoa vyeti 19,926 tu vya usajili. Hilo linamaanisha kwamba ni mtu 1 tu kati ya 53 aliyefaulu kusajili gari lake.