TOVUTI YA JW.ORG
Jinsi ya Kunufaika Zaidi na Video Katika Kifaa Chako
Nenda kwenye MAKTABA > VIDEO ili kuona video zote zilizopo. Kuna vipengele kadhaa na kila kipengele kimegawanyika katika vipengele vingine.
Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma
Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma
Video inapoendelea kucheza, unaweza kutokeza alama za kuichezesha kwa kugusa skrini au kwa kusogeza kipanya juu ya video.
Kitufe |
Kazi Inayofanya |
---|---|
Rudi Nyuma 5 |
Video itarudi nyuma kwa sekunde 5 |
Peleka Mbele 15 |
Video itaenda mbele kwa sekunde 15 |
Iliyotangulia |
Ikiwa video ilianza kucheza itarudi mwanzo, au itacheza video iliyotangulia |
Inayofuata |
Itacheza video inayofuata |
Zima Sauti/Rudisha Sauti |
Hutoa sauti au kuirudisha |
Kuza Video/Punguza Video |
Hukuza ukubwa wa video ili kujaza skrini nzima au kuipunguza iwe ndogo ikiwa ilikuwa imejaza skrini |
Tumia Ishara Kwenye Simu-Janja
Kwenye simu-janja (isipokuwa simu za Apple), tumia ishara zifuatazo ili kucheza, kutua, kupeleka mbele, au kurudisha nyuma:
Kusudi |
Ishara |
---|---|
Cheza au Tua |
Gusa kwa vidole 2 |
Rudi nyuma sekunde 5 |
Gusa mara mbili upande wa kushoto wa video |
Peleka mbele sekunde 15 |
Gusa mara mbili upande wa kulia wa video |
Badilisha Mipangilio ya Video
Bofya Mipangilio:
Bofya kitufe cha Maandishi ya Video (Subtitles) ili yatokee au ili kuyatoa ikiwa yanapatikana.
Chagua Kasi (Speed) ili kubadili kasi ya video
Chagua Ubora (Quality) ili kuchagua ubora wa mwonekano wa video. Namba ndogo hucheza video hata Intaneti isipokuwa na kasi. Namba kubwa hufaa skrini kubwa